Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Ilala ataja anachojivunia kwa miaka mitano

Mjema1 DC Ilala ataja anachojivunia kwa miaka mitano

Sat, 20 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Ilala ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Manispaa hiyo, Dkt. Sophia Mjema amesema utekelezaji wa ilani ya CCM kuanzia 2015/20 Manispaa hiyo imekusanya mapato ya ndani kiasi cha shilingi Bilioni 51.

Akisoma taarifa hiyo ya utekelezaji wa ilani kwa Manispaa hiyo, Dkt. Mjema amesema makusanyo hayo yamekaribia lengo iliyojiwekea la kukusanya kiasi shilingi Bilioni 57, ambapo wametekeleza miradi katika sekta ya barabara, afya pamoja na elimu kwa kujenga majengo mapya ya madarasa pamoja na vyoo katika maeneo ya Shule za msingi na sekondari.

Aidha katika kikao hicho kikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Ubaya Chuma likaibuka sakata la watendaji kuomba rushwa wanaosimamia kutunza mazingira baadhi mitaa ya Gerezani Kamata, suala ambalo limetolewa maagizo.

Katika kikao hicho Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo amepokea Madiwani watatu kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa TLP wilaya hiyo ambao wameamua kuungana na chama cha Mapinduzi CCM.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live