Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Hai awashughulikia waliotafuna Sh126 milioni za Saccos

28035 Pic+dc TanzaniaWeb

Tue, 20 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Hai. Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amewataka viongozi wa saba wa Saccos ya Uswaa Mamba iliyopo wilayani hapa kurudisha Sh126 milioni wanazodaiwa kuzitafuna.

Wanaotuhumiwa ni karani wa Saccos hiyo, Jema Mwakatobe na wengine ni Godbless Uroki, Hellen Mtui, Salatiel Kweka, Godwin Kimaro, Japhet Shoo na Grace Massawe.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Uswaa kilichopo Machame, Ole Sabaya aliwataka viongozi hao kurejesha fedha hizo haraka iwezekanavyo na ndani ya siku tatu wamueleze zilipo fedha hizo.

"Staki blaa blaa hapa. Hizi fedha mmezichukua mafichoni na mtazirejesha hadharani, Serikali hii ni ya kutetea wanyonge, hatupendi kuona wananchi wakiteseka," amesema Ole Sabaya.

Aidha amemuagiza, kaimu ofisa ushirika wa wilaya hiyo, Joel Marandu kufuatilia mwenendo wa chama hicho kujua kama kinawanufaisha wananchi.

Marandu amesema tangu alipopata malalamiko ya wananchi kuhusu upotevu wa fedha zao alianza kufuatilia. "Maagizo niliyopewa nitayafuatilia na kuyafanyia kazi" amesema Marandu.

Karani wa chama hicho, Jema Mwakatobe alipohojiwa kuhusu ubadhirifu wa fedha hizo amesema alikuwa akifuata maelekezo ya wajumbe wa bodi.

"Nilipoingia kwenye chama hiki, nilikuwa bado mdogo, sikujua kinachoendelea hivyo nilikuwa naamriwa kusaini," amesema  Mwakatobe.



Chanzo: mwananchi.co.tz