Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Hai amtupa rumande saa 48 diwani wa CCM

Sat, 1 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Hai. Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amemsweka ndani saa 48 , Diwani wa Okaoni (CCM), Moris Makoi na kutengua umiliki wake wa  shamba la kahawa la Nkwansira  lenye ukubwa wa ekari zaidi ya 500.

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara, uliofanyika Kijiji cha Nkwansira, DC huyo amesema mwekezaji huyo ambaye ni Diwani ameshindwa kuendeleza shamba hilo na kusababishia serikali hasara kwa kutokulipa kodi. Aidha amesema mwekezaji huyo amekua akiwanyanyasa wafanyakazi katika shamba hilo na kuwanyima mishahara. "Kuanzia leo nimetengua maamuzi ya kikao cha wajumbe 31 waliopitisha na kummilikisha shamba hili mwekezaji huyu hivyo, simtambui pamoja na shughuli zake zote ndani ya wilaya hii,"amesema Mkuu huyo. Mkuu huyo amechukua hatua hiyo, baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi wa Kijiji hicho wakimlalamikia mwekezaji huyo kutokana na matumizi mabaya ya shamba hilo ambalo ameshindwa kuliendeleza na badala yake kulibadilisha matumizi. Pia, amesema amekua akikwepa kodi na hajawahi kuona kumbukumbu zozote za kulipa kodi kwa mwekezaji huyo na kwamba hamtambui. "Sina kumbukumbu zozote za mwekezaji huyu na simtambui katika wilaya hi,"amesema Sabaya. "Haiwezekani shamba hili ambalo amepewa na serikali kulima kahawa alitumie kulishia mifugo na kuotesha maharage,"amesema.

Wakizungumzia kuondolewa kwa mwekezaji huyo, wananchi wa kijijini hicho wamefurahishwa na uamuzi ya mkuu huyo na kuomba shamba hilo lirudi mikononi mwa wananchi. Mmoja wa wanakijiji hao, Remani Ulomi amemsema shamba hilo lingeweza kutoa ajira nyingi kwa vijana kwani tangu mwekezaji huyo apewe eneo hilo ameshindwa kutoa ajira kwa vijana hao. "Shamba hili limekua pori, ameshindwa kuliendeleza na ajira hapa hatuna zaidi shamba hili limejaa kila ina ya wanyama, tunaomba shamba hili lirudi mikononi mwetu hatumtaki mwekezaji huyu"amesema Hata hivyo, amemuagiza Kaimu Ofisa ushirika wa Wilaya hiyo, Joel Marandu kutoa ekari 10 kwa wananchi hao na utekelezaji wake uanze mara moja ili wananchi hao wanufaike na ardhi yao.



Chanzo: mwananchi.co.tz