Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Gondwe awaomba radhi wananchi kukosa maji

Thumb 1661 800x420 0 0 Auto DC Gondwe awaomba radhi wananchi kukosa maji

Tue, 25 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe amewaomba radhi Wananchi wa Wilaya hiyo kutokana na kukosa huduma ya maji katika baadhi ya maeneo ikiwemo Boko, Bunju na Mbezi.

DC Gondwe ameyasema hayo wakati akizungumza na wakazi wa maeneo ya Boko National Housing, huku akisema kwamba tayari Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametenga fedha Tsh. Bilioni 65 za miradi ya maji katika Wilaya hiyo.

"Rais Samia ameleta fedha na zimeanza kutumika Tsh. Bilioni 65 kwa ajili ya maeneo ya Kinondoni ikiwemo Boko National Housing ambapo mradi huo utawanufaisha, ndio maana ikawa emergency nikaona isiwe tabu nije mwenyewe nikimbie huku niongee na nyinyi kwa sababu naifahamu hii miradi.”

“Niwaombe radhi Watu wote wa Boko National Housing kwa kutopata taarifa ya nini kimetokea kwa wale ambao wameunganishiwa maji halafu hayafiki.”

"Mtuwie radhi maana utu uzima bhana kuomba radhi ni jambo jema, naomba mtuwie radhi kwamba taarifa za yakifungwa maji huku hayaji, hiyo taarifa ya Kitaalamu haikutolewa, kwa dhati kabisa nakiri kosa haikutolewa.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live