Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe amewataka wamiliki wa bar na kumbi za starehe kufanya biashara kulingana na vibali wanavyopewa na Manispaa.
Ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali ya Kijamii ndani ya Wilaya ya Temeke.
Akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Moringe Kata ya Mbagala, Gondwe amesema wamiliki wote wanatakiwa wafuate vibali vyao kama walivyoelekezwa na Manispaa ili kuondoa kero kwa wananchi wanaoishi maeneo ya karibu.
Gondwe amesema, kila kumbi ya starehe ina kibali chake kuna waliopewa vya kukesha hadi asubuhi, kuna wengine wamepewa mwisho muda fulani ila wapo wanaokikuka na ni kosa kisheria.“Kuna kumbi zinapiga muziki hadi asubuh wakiwa hawana vibali hivyo na wanatoa kero kwa wananchi kuna wengine ni wagonjwa, wanataka kupumzika na hili suala nataka watendaji wa mtaa mlifanyie kazi sitaki kusikia lawama tena za wananchi,” DC GondweGondwe amesema, kama mmiliki amepewa kibali cha kupiga muziki hadi asubuh lakini amekuwa anashindwa kufuata masharti yanayotakiwa na kama Manispaa tukiona mtu anafanya hivyo tutamnyang’anya kibali hicho.DC Gondwe amewataka maafisa Mazingira wa Kata kusimamia mazingira ipasavyo na kuwachukulia hatua kali za kisheria wamiliki wa Viwanda vinavyotiririsha maji machafu kwenye makazi ya wananchi.Hilo, ni kutokana na wananchi wa Kata ya Mbagala kulalamika utiririshwaji wa maji machafu kutoka katika viwanda vilivyopo karibu na maeneo ya wananchi kikiwemo Kiwanda cha Sabuni.Aidha, ametoa maagizo hayo kwa viwanda hivyo kuacha haraka tabia hiyo.Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe akizungumza na wananchi wa kata ya Mbagala baada ya kupokea malalamiko ya kumbi za starehe kupiga muziki mkubwa na kuwa kero kwa wananchi sambamba na uharibifu wa mazingira kutoka kwenye Viwanda.