Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Geita aingilia kati wananchi kugoma kuzika kijana aliyedaiwa kufariki kwa kipigo cha polisi

48840 Geitapic

Wed, 27 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Geita. Mkuu wa Wilaya ya Geita,  Josephat Maganga amewasili katika kijiji cha Nyakafuro kuzungumza na wananchi baada ya kugoma kuzika mwili ya Jackson Charles  anayedaiwa kufariki dunia baada ya kupigwa na polisi.

Licha wananchi kudai Jackson ameuawa kwa kipigo, polisi imebainisha kuwa marehemu alikuwa mgonjwa.

Akizungumza leo jioni Jumanne Machi 26, 2019 Maganga amedai Serikali imesikitishwa na kifo hicho na kwamba katika eneo hilo imani ya wananchi kwa jeshi la polisi imetoweka

Amesema kijiji hicho chenye wananchi zaidi ya 30,000 kina askari watatu pekee hivyo utoaji wa huduma ni mgumu.

Akizungumza katika mkutano huo baba wa marehemu, Charles Sengerema amesema licha ya polisi kudai mtoto wake ana kifafa lakini tangu alipozaliwa hajawahi kuwa na ugonjwa huo.

Sengerema amesema licha ya mwanaye kulazwa hospitali tangu Machi 19, 2019 hakupewa huduma yoyote zaidi ya kuongezewa maji chupa saba.

Amesema mwanaye aliendelea kuwa chini ya ulinzi wa polisi licha ya kutojitambua huku akiwa amefungwa pingu.

Amesema baada ya mwanaye kufariki na kutaka kuchukua mwili kwa ajili ya maziko, marehemu alikutwa na majeraha kuanzia kichwani, mgongoni na kiunoni.

Soma Zaidi>>DC Geita aingilia kati wananchi kugoma kuzika kijana aliyedaiwa kufariki kwa kipigo cha polisi

 Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi



Chanzo: mwananchi.co.tz