Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC DODOMA: Wazazi acheni visingizio vya sare na madaftari

9af55150c933b56eb628ac7201f37aec.jpeg Wazazi acheni visingizio vya sare na madaftari

Wed, 2 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri amewaagiza wazazi na walezi wote wenye watoto waliofaulu darasa la saba wawapeleke shuleni na kuacha visingizio vya ukosefu wa sare na madaftari.

Alisema hayo juzi wakati akizungumza na wananchi kwenye kufanya usafi wa mazingira katika Kata ya Kikuyu Kusini jijini hapa.

Aliwataka wazazi na walezi ambao watoto wao wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza kuhakikisha watoto hao wanapelekwa shuleni na kuanza masomo.

Shekimweri alisema Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mikoa yote hapa nchini na kwa Wilaya ya Dodoma karibu madarasa 143 tayari yameshajengwa na kukamilika na kuwekewa mahitaji yote yanayohitajika kwa wanafunzi na walimu.

“Hivyo hakuna kikwazo kwa wazazi na walezi wote wenye watoto ambao bado wamewaweka majumbani kwa kisingizio cha kushindwa kuwapeleka shule kutokana na kukosa sare, kinachotakiwa wapelekwe kwanza na sivyo vinginevyo,” alisema.

Alisema suala la sare siyo sababu ya kutowapeleka shule watoto waliochaguliwa kuanza elimu ya kidato cha kwanza wakati Rais ametoa fedha nyingi ili wote wasome na kusiwepo hata mojawapo aliyefaulu akashindwa kupata elimu kwa visingizio vya kukosa madarasa.

"Ninatoa agizo kwenu nyinyi wazazi na walezi wenye watoto mnaowaweka majumbani kwa kisingizio cha kukosa sare na mahitaji mengineyo, msiwakwamishe watoto wenu hao, badala yake wapelekeni mashuleni masuala ya sare na madaftari hayo yatafuata baadaye," alisema.

Mkuu huyo wa wilaya aliwataka wananchi wa Dodoma kuwa na tabia ya kupanda miti na kuitunza kwenye maeneo yao wanayoishi ili waweze kutunza mazingira na kuifanya Dodoma kuwa ya kijani wakati wote.

Awali akizungumza kwenye usafi wa mazingira katika kata hiyo ya Kikuyu Kusini, Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru alionya wananchi kuacha tabia ya ujengaji holela na uharibifu wa mazingira, badala yake amewataka kufuata sheria zilizowekwa na jiji hilo.

Mafuru alisema halmashauri ya jiji kamwe haitawafumbia macho na kuwaonea huruma wale wanaojenga na kuharibu mazingira, hivyo wananchi wafuate taratibu na sheria zilizowekwa pindi wanapohitaji kujenga.

Aliwataka wakazi wa kata zote za Jiji la Dodoma kutoa ushirikiano katika suala zima la ufanyaji wa usafi wa mazingira,hivyo wananchi wafuate taratibu na sheria zilizowekwa pindi wanapohitaji kujenga.

Aliwataka wakazi wa kata zote za Jiji la Dodoma kutoa ushirikiano katika suala zima la ufanyaji wa usafi wa mazingira, badala ya kusubiri kushinikizwa kwa kusimamiwa na sheria ikiwemo ya kulipishwa faini.11

Chanzo: www.tanzaniaweb.live