Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Chato awataka vijana kupunguza kunywa pombe

POMBE Jk DC Chato awataka vijana kupunguza kunywa pombe

Wed, 9 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa wilaya ya Chato Martha Mkupasi amewataka vijana wilayani humo kupunguza matumizi ya Pombe ili kujiepusha na hatari ya kukumbwa na magonjwa ya Moyo na shinikizo la damu kwa sababu ni moja ya kisababishi vya magonjwa hayo

Mkupasi ameyasema hayo wakati wanahitimisha huduma za kibingwa za upimaji na matibabu ya Ugonjwa wa Moyo yaliyokuwa yanafanyika katika Hospitali ya kanda ya rufaa ya Chato na kuonekana Pombe ni moja ya visababishi vya maradhi ya Moyo

"Vijana tunaita kumwagilia Moyo, unaweza ukasema nina mawazo makubwa ngoja niende mahali nikamwagilie Moyo, kumbe ndio unajiua kabisa, unamwagilia moyo siku ya kwanza ujala kitu, siku ya pili ya tatu mwezi mzima, unatafuta matatizo"

"Kwahiyo ile huduma wametupatia hapa namna bora ya kuishi, imetusaidia pia kuelewa lakini pia, sisi tutakuwa ni mabalozi wazuri kutoa taarifa hizi kwa wale ambao hawakufanikiwa kufika hapa, lakini hata waliofika hapa, nina amini kwamba, watakuwa ni mabalozi wazuri kwa ajili ya wanachi ambao wanakwenda kukutana nao majumbani kwao na maeneo mengine wanapokwenda kufanyia kazi", alisema Mkupasi.

Mkuu wa idara ya utafiti na mafunzo Taasisi ya Moyo ya jakaya Kikwete Petro Pallangyo anasema zaidi ya watu 500 wamejitokeza katika upimaji na tatizo lililoonekana kwa watu wazima ni shinikizo la Damu ambao linasababishwa na mtindo wa maisha.

"Tunasema kuna visababishi vitano vikubwa vyaupande wa namna ya kuishi vikijumuisha, uvutaji wa sigara, unywaji wa Pome kupindukia, uzito mkubwa, ulaji usiofaa na kutofanya mazoezi vitu hivi kutokana na maisha kuboreka vinafanya watu wngi sana wanakuwa na tabia bwete na matokeo yake magonjwa haya yasiyo ya kuambukiza hususani shinikizo la damu high blood pressure, linaongezeka katika jamii zetu", alisema Pallangyo.

Mwakilishi wa mgodi wa dhahabu wa GGML Lauren Pima anasema wamefarijika kuwa sehemu ya zoezi la upimaji na upatiwaji wa matibabu kwa wananchi waliojitokeza kwenye zoezi hilo.

"Tumefurahi kwamba zoezi hili limevutia watu wengi, kutoka maeneo ya Geita lakini tumefarijika kuona maeneo ya Bukoba na sehemu zingine, kwahiyo hii inathibitisha kabisa kwamba ushirikiano wetu mzuri kati ya sekta binafsi na serikali umekuwa na matokeo chanya kwahiyo hii public private patnership ni jambo zuri kwakweli ambalo tunaona kuna haja kuendeleza kwa maslahi mapana ya maendeleo ya watu wote", alisema Pima.

Pamoja na zoezi hilo kufika tamati lakini huduma hizo zitaendelea kupatikana katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Chato kwani wataalam kwenye Hospiyali hiyo wamejengewa uwezo na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live