Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Bulembo awaonya maafisa usafirishaji

DC Bulembo Awaonya Maafisa Usafirishaji DC Bulembo awaonya maafisa usafirishaji

Thu, 21 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa wilaya ya Kigamboni, Halima Bulembo amewaonya maafisa Usafirishaji kwa kutumia pikipiki maarufu kama Bodaboda kuacha tabia ya kutembea na wanafunzi na kuwaharibia malengo kwakuwapa ujauzito.

DC Bulembo ametoa onyo hilo katika Kata ya Kigamboni jijini Dar es Salaam wakati akihitimisha ziara yake ya 'DC Barabarani' ya kusikiliza na kutatua kero za mdereva katika wilaya hiyo wakiwemo Bodaboda, Bajaji na Daladala, aliyoifanya katika kata tisa za Kigamboni.

Aidha amesema onyo hilo limetokana na uwepo wa baadhi ya madereva bodaboda kuripotiwa kuwapa ujauzito wanafunzi zaidi ya watatu, ambapo amewataka kuwatunza na kuwachukuliakama dada zao.

Katika hatua nyingine, amewataka madereva kutii sheria bila shuruti pindi wanaposimamishwa na trafiki ili kupunguza malalamiko ya kunyanyaswa na askari kutokana na ukaidi wa kutii sheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live