Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Bulembo: Shule zinazotoa chakula zinafaulisha kuliko zisizotoa

Halima Bulembo Mkuu wa Wilaya mpya ya Kigamboni, Halima Bulembo

Thu, 26 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Halima Bulembo amewataka Wazazi na walezi kuhakikisha wanachangia chakula shuleni, ili watoto waweze kupata Chakula pindi wawapo shuleni.

Wito huo ameutoa wakati wa ziara yake ya kata kwa Kata, ya kusikiliza na kutatua kero pamoja na kukagua miradi ya Maendeleo iliyopo Wilayani humo.

Bulembo alieleza kuwa walaka wa elimu namba tatu mwaka 2016, unawataka Wazazi na Walezi kushirikiana na Uongozi wa shule kutengeneza utaratibu wakutoa chakula kwa shule za kutwa na bweni.

Mkuu wa Wilaya huyo ambaye kwa sasa amehamishiwa Wilaya ya Kigamboni Mkoa wa Dar Es Salaam, alisisitiza kuwa tafiti zinaonesha kuwa shule zinazotoa chakula shuleni watoto wanafaulu kuliko ambazo hazitoa chakula Cha mchana kwa wanafunzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live