Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Bagamoyo ataka weledi watumishi wa umma

Zai Dc.jpeg DC Bagamoyo ataka weledi watumishi wa umma

Fri, 25 Jun 2021 Chanzo: ippmedia.com

Zainabu ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akiongea na wakuu wa idara mbalimbali kutoka katika Halmashauri za Bagamoyo pamoja na Chalinze kwa lengo la kujadili mipango ya kimaendeleo muda mfupi baada ya kukabidhiwa Ofisi.

"Lengo langu katika kikao hiki ni kukutana na wakuu wa idara ambao nina imaniĀ  ndio wataweza kunisaidia katika kutekeleza majukumu yangu ya kila siku kikubwa ni lazima kuwe na nidhamu katika suala zima la uwajibikaji ikiwa niĀ  pamoja na kutenda haki kwa kila mmoja," amesema Zainabu.

Aidha, Zainabu amewataka watumishi hao kuhakikisha wanaachana na tabia ya kukaa maofisini na badala yake wabadilike kwa kuwatembelea Wananchi ili kubaini kero zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, Kasilda Mgeni, pamoja na wakurugenzi wa Halmashauri hizo wameahidi ushirikiano kwa Mkuu huyo wa Wilaya na kufuata maagizo aliyoyatoa.

Chanzo: ippmedia.com