Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC Arusha ampinga Gambo ubebaji abiria katika bodaboda

2171d2f9b9055e880640b38c0d736fb6 DC Arusha ampinga Gambo ubebaji abiria katika bodaboda

Thu, 17 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa wilaya ya Arusha, Kenan Kihongosi amekataa hoja ya Mbunge wa Arusha Mjini, Mrisho Gambo aliyotaka waendesha pikipiki ya matairi matatu ‘Bajaji’ waruhusiwe kubeba abiria hadi wanne na kumtaka Mbunge huyo kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani.

Akizungumza kwenye Mkutano wa waendesha Bajaji na pikipiki jijini Arusha ulioitishwa na Jeshi la Polisi kwa lengo la kuwakumbusha Sheria za usalama barabarani na kusikiliza kero zao, Mkuu huyo alidai kuwa hoja za Mbunge huyo zinakiuka sheria za usalama barabarani.

Kihongozi alisema kuwa Mbunge huyo hapaswi kutetea hoja ambayo anajuwa inavunja sheria na kuhatarisha usalama wa raia, na kwamba ni vyema waendesha pikipiki kufuata sheria.

“Hoja ya Mbunge tumeielewa na tunamheshimu sana, lakini afuate sheria za nchi, hatuwezi kuruhusu hoja ambayo inahatarisha usalama wa raia,” alisema.

Awali Gambo akizungumza kwenye mkutano wa waendesha Bajaji na pikipiki jijini Arusha ulioitishwa na jeshi la polisi kwa lengo la kuwakumbusha Sheria za usalama barabarani na kusikiliza kero zao, aliomba waendesha Bajaji waruhusiwe kupakia abiria wanne kinyume na sheria jambo ambalo lilipingwa vikali na mkuu hiyo wa wilaya.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Salumu Hamduni alisema hivi karibuni kumeibuka matukio ya uhalifu wa kutumia bodaboda katika kutekeleza uhalifu,ndio maana tumeitisha kikao hiki ili kuzungumzia changamoto zinazojitokeza.

Chanzo: habarileo.co.tz