Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DAWASA yawaondoa wasiwasi watumiaji maji (+Video)

Video Archive
Sat, 23 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imekiri kupata taarifa za tatizo la upatikanaji wa maji katika baadhi ya maeneo unaosababishwa na msukumo mdogo kutoka katika chanzo cha maji cha Ruvu Chini.

Dawasa imesema tatizo hilo limesababishwa na upungufu wa maji katika mitambo ya kuzalisha maji ambayo imelazimu Mamlaka kupunguza uzalishaji maji kutoka lita milioni 270 hadi lita milioni 210 kwa siku.

Uwezo wa kuzalisha maji kwa siku ni lita milioni 520, hata hivyo kutokana na upungufu wa maji katika chanzo cha mto Ruvu, Dawasa inazalisha lita milioni 460 sawa na upungufu wa lita milioni 60 kwa siku.

“Kupungua kwa kina cha maji katika chanzo cha maji kumetulazimu kuhamisha maji kutoka Ruvu Juu ili kuhudumia baadhi ya maeneo yaliyokuwa yakihudumiwa na mtambo wa Ruvu Chini,” Cyprian Luhemeja Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa amewaambia waandishi wa habari na kukiri kuwa hatua hiyo imesababisha baadhi ya maeneo kuchelewa kupata maji kwa angalau siku moja hadi mbili.

“Tuwaondoe wasiwasi, Dawasa tumejipanga na tuna maboza kwa wale ambao watakuwa na changamoto kubwa basi tutawapelekea maji.” Uzalishaji katika mtambo wa Ruvu Juu bado ni Lita milioni 127 kwa siku, Mtambo wa Wami pia unazalisha lita milioni 7.3 na chanzo cha mtoni pia kinazalisha lita milioni 6.8 hadi 7 kwa siku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live