Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DAWASA yaboresha huduma unyonyaji majitaka kwa bei nafuu

WhatsApp Image 2021 04 09 At 11.05.49.jpeg DAWASA yaboresha huduma unyonyaji majitaka kwa bei nafuu

Fri, 9 Apr 2021 Chanzo: ippmedia.com

DAWASA imesema, miongoni mwa jukumu yao ni pamoja na kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama kwa wananchi wanaowahudumia, ili kuwaepusha na magonjwa ya mlipuko.

Afisa Biashara, Idara ya Majitaka DAWASA, Daniel Mauma amesema, wana vifaa bora vya kutolea huduma hiyo ikiwemo magari ya kisasa lenye uwezo kunyonya lita za ujazo 18,000 ndani ya dakika sita mpaka 10, kwa bei nafuu.

Mauma, amesema, gari lenye ujazo wa lita 5,000, hunyonya kwa Sh.50,000; lita 9000 kwa Sh.100,000 na gari kubwa la lita 18,000 kwa Sh.150,000 kwa majumbani na Sh.180,000 sehemu za biashara.

"Huduma hii imeanza tangu mwezi Machi mwaka huu na tunapokea oda za wananchi kupitia namba yetu ya simu ambayo ni 0735451879" amesema Mauma

Deogratius Mrema, mmoja wa wananchi waliopata huduma hiyo, amesema, DAWASA imefanya jambo jema kuanzisha huduma hiyo kwani ni ya gharama nafuu ukilinganisha na watoa huduma wengine.



"Tunafurahishwa na upatikanaji wa huduma hii, kwa kuwa ni ya gharama nafuu na hupatikana muda wote," amesema Mrema

Mrema amesema, kutokana na gharama ya DAWASA kuwa nafuu, itawafanya wananchi wengi kuitumia na kuepuka kutiririsha majitaka katika makazi ya watu na kusababisha magonjwa ya mlipuko.
Chanzo: ippmedia.com