Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DAS Njombe: Ualimu sio kimbilio kwa waliofeli

Njo1 Ed.jpeg DAS Njombe: Ualimu sio kimbilio kwa waliofeli

Fri, 26 Nov 2021 Chanzo: ippmedia.com

KATIBU Tawala Wilaya ya Njombe Emmanuel George, amesema Jamii inapaswa kuondoa dhana potofu iliyojengeka kwa watu wengi kuhusu taaluma ya ualimu kwamba ni ya watu waliofeli.

"Fani ya ualimu sio kimbilio la waliofeli darasani, lazima iheshimiwe, hii ni taaluma ambayo haipaswi kudharauliwa nawaomba sana walimu waheshimiwe ili watuandalie kizazi kilicho bora" amesema George.

Zoezi la kuwajengea uelewa wa kimaadili walimu linafanyika kote nchini ikiwa ni kuwarejesha kwenye maadili baadhi ya walimu wanaoonekana kwenda kinyume na maadili ya taaluma hiyo, kwa Wilaya ya Njombe semina hizo zinafanyika Makambako, Njombe pamoja na Lupembe.

Chanzo: ippmedia.com