Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Choo chawaweka matatani watu hawa

Choo Ytes Choo chawaweka matatani watu hawa

Thu, 6 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameagiza kukamatwa na kufanyiwa uchunguzi kwa wasimamizi wote walioshindwa kusimamia ujenzi wa matundu 14 ya vyoo yaliyo gharimu kiasi cha shilingi milioni 36 katika shule ya msingi Mtipwili iliyopo wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma

Akiwa katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma katika ukaguzi wa miradi ya uboreshaji miundombinu ya shule za msingi (BOOST) mkuu wa mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomasi amesikitishwa na usimamizi mbovu wa ujenzi wa matundu 14 ya vyoo katika shule hiyo iliyopo kata ya Mtipwili wilaya ya Nyasa mkoni Ruvuma

Ujenzi huo uligharimu kiasi cha shilingi milioni 36 ambapo mkuu wa mkoa wa Ruvuma ameagiza kukamtwa na kufanyiwa uchunguzi wasimamizi wote ambao wameshindwa kusimamia mradi huo.

Kwa upande wao wananchi wa kijiji cha Mtipwili wamesema kitendo cha kushindwa kusimamia mradi huo ni kibaya na licha ya serikali kutoa milioni 36 katika ujenzi wa matundu 14 ya vyoo vya shule hiyo lakini pia wananchi walichangishwa kiasi cha shilingi elfu 5 kwa kila kaya pamoja na kuchimba mashimo ya vyoo hivyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live