Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chongolo kuleta neema ya maji Rukwa

Chongolo Atua Mpanda, Aanza Na Umeme.jpeg Chongolo kuleta neema ya maji Rukwa

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amewahakikishia Wananchi wa kijiji cha Palamawe wilayani Nkasi mkoani Rukwa kuwa atakwenda kusaidia kutafuta shilingi Milioni 500 kwa ajili ya kuboresha mtandao wa maji katika kata mbili za Myula na Kate wilayani humo.

“Nimesikia hapa inatakiwa tutafute fedha kama Milioni 500 ili kuboresha mtandao wa upatikanaji maji. Mtalaamu anasema tukipata shilingi 500 Milioni mtandao wa maji kwa hizi kata mbili utaboreshwa na utatoa maji vizuri, sasa nalichukua hilo la kwenda kusukuma fedha Sh.milioni 500 ili ziweze kuboresha mtandao wa maji hapa,” Amesema Ghongolo na kuongeza kuwa

“Wao wabakie na jukumu la kuchimba visima hivyo viwili kwenye maeneo mawili waliyosema na kutafuta fedha waniachie mimi na Mbunge wenu. Sisi tunaenda kuhangaika nalo".

Chongolo ambaye yupo mkoani Rukwa akitokea mkoa wa Katavi kuendelea na ziara yake ya kuhamasisha uhai wa CCM, kusikiliza changamoto za Wananchi na kukagua miradi ya maendeleo inayotokana na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 - 2025, alizungumzia changamoto hiyo baada ya kusikiliza malalamiko ya Wananchi waliodai kuwa maji kwa sasa hayatoshelezi kwa sababu mradi uliopo umekuwa wa muda mrefu.

Akizungumzia miundombinu ya barabara, Chongolo ametumia nafasi hiyo kumsimamisha Meneja Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) ili kutoa maelezo kuhusu hatua zinazochukuliwa kuboresha barabara ambazo zimelalamikiwa na Wananchi kuwa hazipitiki nyakati zote ambaye katika maelezo yake alieleza kuwa kila mwaka wamekuwa wakifanya maboresho ya barabara zote korofi kwa kuweka zege katika maeneo ya vilima vikali pamoja na makaravati.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live