Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chongolo awataka TANROADS Morogoro kujitathmini

Chongolo New Chongolo

Wed, 1 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Daniel Chongolo amemtaka Meneja wa Tanroads Mkoa wa Morogoro kujitathimini kuhusu Barabara ya Kidatu Kilombero Ujenzi ambayo ilianza Mwaka 2017 chini ya Kampuni ya Ukandarasi ya Reynolds construction kutoka Nigeria Lakini hadi Leo bado haijakamilika

Aliongea hayo leo Mkoani Morogoro mbele ya Wananchi wa Wilaya hiyo ya Kilombero kwenye daraja la Mto Kilombero

Amesema Barabara hiyo mbayo inaonganisha Wilaya ya Kilombero na Kilosa ni muhimu kwa Wananchi hivyo ujenzi wake unatakiwa kumalizika haraka

"Ninemsikiliza Meneja wa Tanroads Mkoa wa Morogoro kuwa hadi mwezi wa kumi Barabara hii itakuwa imekamilika Kwa asilmia mia moja na nimemwambia nitakuja tena hapa,"

Na kuongeza" Sasa meneja ni Bora ukasema ukweli kama zipo changamoto tuzitatue mapema ikiwa tofauti na hapo, tutaangalia mwingine anayetosha ili mamba yaende" Alisema Katibu Mkuu

Awali Mbunge wa Kilombelo Abubakari Asenga alimlalamikia ucheleweshwaji wa ujenzi wa Barabara hiyo ya Kidatu Kilombelo ambao Ujenzi wake ulianza Mwaka 2017.

Akitoa maelekezo ya mradi meneja wa Tanroads Mkoa wa Morogoro Alinanuswe Kyamba amesema kuwa ujenzi wa Barabara ulitakiwa kukamilika mwaka 2020 Lakini Barabara kutokana na changamoto za kukosa vibali vya wafanyakazi na msamaha wa kodi kwa baadhi ya vitendoa kazi imekwamisha kukamilika kwa barabara hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live