Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chongolo atoa maagizo pori la akiba Dodoma

Chongolo Pic Data Chongolo atoa maagizo pori la akiba Dodoma

Tue, 20 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ametoa wito kwa Wananchi wa maeneo mbalimbali wilayani Kondoa mkoani Dodoma wanaopakana na Pori la Akiba la Mkungunero, kuheshimu taratibu za kisheria za nchi na iwapo kuna sheria inayohitaji marekebisho basi utaratibu uliowekwa kufanya mabadiliko ufuatwe.

Chongolo ameyasema hayo wakati akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Kinyasi kata ya Kinyasi (Bwawani) baada ya kutembelea ujenzi wa mradi wa shule ya msingi Kinyasi, Bwawani, iliyoanzishwa kwa nguvu za Wananchi kwa kuchanga shilingi Milioni nane na Serikali kutoa zaidi ya shilingi Milioni 490.

Alitoa kauli hiyo baada ya kupokea malalamiko ya Wananchi hao kuhusu mgogoro wa muda mrefu juu ya mpaka wa pori hilo la akiba la Mkungunero.

"Sheria lazima ibaki kuwa sheria na tunapotaka kubadilisha sheria lazima twende kwenye mchakato wa kubadili sheria,” amesema Chongolo.

Katika ziara hiyo yenye lengo la kukagua, kusimamia na kuangalia maendeleo ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025 pamoja na kuimarisha uhai wa Chama Cha Mapinduzi, Katibu Mkuu wa CCM ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Sophia Mjema pamoja na Katibu wa NEC Oganaizesheni Issa Haji Ussi Gavu.

Leo Juni 20, 2023 Katibu Mkuu huyo wa CCM anatembelea wilaya ya Chemba, ukiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya siku nane mkoani Dodoma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live