Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chongolo ashtuka kasi ya mimba za utotoni Songwe

WhatsApp Image 2022 05 25 At 3 Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutokana na ongezeko la mimba za utotoni, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo ametangaza msako mkali kwa watakaobainika kuhusika.

Chongolo ametangaza msako huo leo Jumanne Aprili 30, 2024 wakati akizungumza na wananchi wilayani Ileje ikiwa ni mwendelezo wake ziara ya kukagua miradi ya maendeleo.

Amesema mkoa huo unaongoza kitaifa kwa kuwa na asilimia 45 ya mimba za utotoni huku takwimu zikionesha miezi minne kuanzia Januari hadi Aprili mwaka huu watoto 170 wameripotiwa kupata ujauzito.

Chongolo amesema takwimu hizo hazifurahishi hata kidogo na kwa kuwa kapewa dhamana ya kusimamia Songwe, atahakikisha wanashirikiana na timu ya usalama mkoa na wilaya kushughulika na wanaume wote wanaowapa mimba wanafunzi hao.

"Hapa nipo Wilaya ya Ileje ambayo kimkoa inaongoza kwa mimba za utotoni, kamanda wa polisi upo hapa hakikisha wakaidi wanakamatwa, mkuu wa Takukuru upo hakikisha rushwa haifanyiki kwa watakaokamatwa, mkuu wa gereza upo utaletewa sana wanaowapa mimba watoto," amesema Chongolo.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Gallus Hyera amewatangazia kiama wanaume wenye tabia za kujihusisha kimapenzi na watoto akieleza kuwa jeshi hilo litahakikisha linashughilika nao kutokana na tabia ya kukatisha ndoto za wanafunzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live