Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chiku Gallawa awabeza waliofurahia kustaafu kwake

10502 Chiku+pic TanzaniaWeb

Tue, 7 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbozi: Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa amesema waliofurahia kustaafu kwake wamepata hasara kwani anayeshika nafasi yake ni mkali kuliko yeye.

Ametoa kauli hiyo leo Agosti 7 katika kikao cha makabidhiano kilichofanyika katika Ukumbi wa halmashauri ya Mbozi.

Amesema kuna wahalifu waliofurahia kuondoka kwake wakidhani wataitumia nafasi ya mabadiliko kuendeleza uhalifu.

"Kama ni suala la kuwaendesha watu kijeshi nafuu yangu nilipita maeneo mengi nikapozwapozwa huko, lakini mkuu mpya ni kamanda kweli kweli, hivyo wale wajipange la sivyo mtaachwa." amesema Gallawa.

Mkuu wa mkoa wa Songwe Nicodemus Mwangela amewasili katika ofisi yake mpya leo asubuhi.

 

Hakuweza kuzungumza lolote  kwa kuwa muda huu anaendelea kupokea taarifa ya mkoa katika kikao maalumu kilichohusisha wafanyakazi wa mkoa Songwe Wakuu wa wilaya zote za mkoa huu,wakurugenzi watendaji na mwenyekiti wa halmashauri ya Mbozi.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz