Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chifu mkuu: JPM anatuthamini, amsimika mwingine

539d2c398ec67248ef671139c75024e5 Chifu mkuu: JPM anatuthamini, amsimika mwingine

Fri, 13 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

CHIFU Mkuu wa Kanda ya Kati mkoani Dodoma, Mazengo wa Pili, amemsimika Luwawo Samwel kuwa Chifu wa Kata ya Mtumbulu mkoani hapa.

Akizungumza baada ya kumsimika chifu huyo, Mazengo wa Pili alimshukuru Rais John Magufuli kwa kuthamini mchango wa viongozi hao wa kimila nchini.

Luwawo aliyesimikwa uchifu katika kata hiyo alisema atakuwa mwaminifu katika eneo lake na kuwaheshimu watu wake wote bila ya kujali rangi ya mtu.

Akitoa historia ya wenyeji wa Matumbulu iliyotungwa na Richard Luwawo, Alfred Wiliam Malogo alisema jina la Matumbulu linatokana na mti ulioitwa Munhumbulu na kuna usemi unaosema kwamba, wanyeji wa matumbulu ni watu wa milango mingi.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo Utamaduni, Sanaa na Michezo aliyekuwa mgeni rasmi katika kusimikwa kwa chifu huyo, Leah Kihimbi, alisema jukumu la kulinda, kukuza na kuendeleza utamaduni ni la wanajamii wenyewe kwa sababu utamaduni ni maisha.

Naye Diwani wa Kata ya Matumbulu, Chibago Samson aliipongeza serikali kwa kutambua mchango wa machifu hapa nchini huku akisema kuwa chifu huyo aliyesimikwa watashirikiana naye kwa kazi mbalimbali ili kusaidia changamoto zinazojitokeza katika jamii hiyo.

Chifu huyo amesimikwa katika eneo la babu yake Luwawo aliyewahi kuwa chifu katika Kata ya Matumbulu zaidi ya miaka 40 iliyopita.

Chanzo: habarileo.co.tz