Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chanzo migogoro ya ardhi Kilosa chatajwa

67072 Migororo+pic

Wed, 17 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Meneja mradi wa kuleta mageuzi katika sekta ya mkaa Tanzania (TTCS) wa Shirika la kuhifadhi misitu asili Tanzania (TFCG),  Charles Leonard amesema migogoro maeneo ya vijiji ni chanzo cha baadhi ya vijiji wilayani Kilosa kutokuwa na mpango bora wa matumizi ya ardhi.

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Julai 16, 2019 wilayani Kilosa katika mkutano wa madiwani na wadau wa misitu.

Amesema lengo la mradi huo ni kuboresha usimamizi wa misitu hasa rasilimali zilizopo katika ardhi za vijiji vya Wilaya hiyo.

Amebainisha kuwa wilayani Kilosa vijiji 20 vilivyopo katika mradi huo vimewezeshwa katika usimamizi shirikishi wa misitu jambo litakalosaidia jamii kunufaika na kupunguza ufyekaji wa misitu.

Amesema kati ya vijiji hivyo, 18 vina mpango wa matumizi bora ya ardhi na viwili vya Mvumi na Rudewa-Gongoni ndio havijaingia katika mpango huo kutokana na mgogoro.

Chanzo: mwananchi.co.tz