Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chanzo cha ajali iliyoua 17 Tanga chatajwa

Qjali Coaster Tanga 33 Ajali iliyoua Tanga

Sat, 4 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi nchini Awadh Haji, amesema chanzo cha ajali iliyotokea wilayani Korogwe na kuua watu 17 umetokana na uzembe wa dereva wa Fuso aliyekuwa akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake na hatimaye kugongana uso kwa uso na Coaster.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamishina Awadh amesema katika tukio hilo limesababisha vifo vya watu 17 ambapo watu nane walifariki papo hapo kwenye eneo la tukio na watu wengine tisa kufariki hospitali huku mejeruhi wakiwa ni 12 ambao wanaendelea na matibabu katika hospital ya Rufaa Bombo.

"Dereva wa Fuso amechangia ajali hii kwa uzembe wa hali ya juu kwa sababu ame-overtake kwenye eneo ambalo lina kona kali pamoja na mwinuko na kupelekea ajali iliyosababisha vifo vya Watanzania wenzetu 17," amesema Kamishna wa Oparesheni Awadh Haji

Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia Februari 4, 2023, na imehusisha Fuso iliyokuwa ikielekea Dar es Salaam na gari ya abiria aina ya Coaster iliyokuwa imebeba mwili wa marehemu kutokea Dar es Salaam kuelekea mkoani Kilimanjaro.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live