Dar es Salaam. Kuenzi mchango wa waanzilishi wake, Chama cha Wahasibu Tanzania (TAA) kimetoa vyeti kimetoa vyeti kwa wenyeviti wake wastaafu na kumtambua marehemu Reginald Mengi.
Akitoa vyeti hivyo, mwenyekiti wa TAA anayemaliza muda wake, Dk Fred Msemwa amesema Dk Mengi alikuwa mhasibu makini aliyesimamia maadili ya taaluma hiyo.
“Wazee wetu walikianzisha chama hiki na wametuachia tukiendeleze kupigania haki zetu huku tukitimiza wajibu kwa jamii,” amesema Dk Msemwa.
Kwa miaka mingi aliyohudumu kwenye baraza la chama hicho, Dk Mengi alikuwa mwenyekiti wa kamati ya maadili.
Dk Msemwa amesema wahasibu wana mchango mkubwa kwenye uchumi wa Tanzania hivyo ni lazima wawe pamoja ili kukumbushana umuhimu wa kutanguliza uzalendo katika utekelezaji wa majukumu sambamba na kutetea na kulinda hadhi ya taaluma yao.
TAA ilianzishwa mwaka 1983 na Hatibu Senkoro akachaguliwa kuwa mwenyekiti wake wa kwanza mpaka mwaka 1987 alipolithiwa na Ernest Massawe aliyekiongoza hadi mwaka 1991.
Pia Soma
- VIDEO: Diamond azungumzia kufunga ndoa na Tanasha
- Kaka yake Lissu ajitenga na uchaguzi mdogo
- Aliyesota miaka 20 jela aoa aliyehukumiwa kifungo cha maisha
Hivi sasa, chama hicho kimemchagua Peter Mwambuja kuwa mwenyekiti wake wa 10 tangu kilipoanzishwa.