Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chalamila hana taarifa za maandamano, asisitiza usafi

Chalamila: Viongozi Wa Dini Muiombee Serikali Chalamila hana taarifa za maandamano, asisitiza usafi

Mon, 15 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema hana taarifa za maandamano ya Chadema yaliyotangazwa kufanyika Junuari 24, mwaka huu akisema anachojua siku hiyo ni ya kufanya usafi.

Akizungumza leo Jumatatu Januari 15, 2024 katika mkutano wake na watendaji wa Serikali kuhusu tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko, Chalamila amesema watu wanahusisha shughuli ya usafiri aliyoitangaza na maandamano ya Chadema ambayo yeye anadai hana taarifa nayo.

Hata hivyo, amesema wakati baadhi ya watu wakihusisha tukio hilo la kufanya usafi na maadamano ya Chadema, yeye hana taarifa hizo kwa kuwa anayepaswa kuzitoa ni Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro.

"Mimi sina taarifa za maandamano na pia shughuli za watu wengine haziwezi kusimamisha shughuli za Serikali, ninachojua siku hizo ni kampeni kabambe ya kufanya usafi," amesema Chalamila.

Aidha, kuelekea Janauri 23 na 24 mwaka huu ambayo ilitangazwa kuwa siku ya usafi utakaohusisha vyombo vya ulizi, Chalamila, amewaonya wananchi wabishi kutoa fedha kwa ajili ya kuzoa taka.

Amesema siku hiyo ni ya usafi kabambe, lakini ana taarifa za baadhi ya wananchi kugomea kutoa tozo ya taka, hivyo kuwaonya kuwa siku hiyo ya usafi watachukuliwa hatua.

Kadhalika Chalamila amesema kuna haja ya kutengenezwa sheria ndogondogo za kusimamia utekelezaji wa utoaji fedha ya kuzoa taka ili atakayekaidi achukuliwe hatua mara moja.

"Kuzolewa taka sio jambo la hiari bali ni la lazima kwa kuwa umezizalisha mwenyewe na zisipotolewa zitaleta magonjwa," amesema Chalamila.

Katika hatua nyingine, ameomba wadau mbalimbali kujitokeza kutoa vifaa vya kufanya usafi siku hiyo ya Januari 23 na 24 huku akitangaza kila wiki usafi utakuwa ukifanyika.

Amesema Januari 20 anategemea kuanza kugawa vifaa vya usafi katika vyombo vya dola.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live