Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chalamila awapa neno waimbaji

06ae7abc2d2c633cefe9ae943ec90b80 Chalamila awapa neno waimbaji

Sun, 25 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WAIMBAJI wa nyimbo za dini mkoani Mbeya, wameaswa kutunga na kuimba nyimbo zenye ujumbe wa kuhimiza uchaguzi wa amani na utulivu na kuliombea taifa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila alitoa wito huo alipokutana na vikundi mbalimbali vya waimbaji wa nyimbo za dini za kikristo na kiislamu kwenye ukumbi wa Mkapa jijini hapa.

Chalamila alisema waimbaji wa nyimbo za dini, wana nafasi kubwa ya kuelimisha na kuhamasisha jamii kupitia uimbaji wao.

Hivyo kipindi hiki ni muhimu wakatoa mchango wao kwa kuhimiza jamii kujikita kwenye kampeni za amani ili kufanya uchaguzi wenye amani na utulivu.

“Mnao uwezo wa kuwafanya waumini wabadili mienendo yao na kumfuata Mungu…hili la kuhimiza watanzania kuwa watulivu wakati wa uchaguzi na hata baada mnaliweza kabisa na ndiyo maana nawaomba mtusaidie.Taifa hili ni letu sote na tungependa kuona amani inaendelea kutamalaki tukiamini kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi,” alisisitiza Chalamila.

Aliwaomba viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini, kuhubiri umuhimu wa amani na ndiyo msingi wa wenye kuwezesha watu kupata fursa ya kuabudu.

Kwa upande wao, waimbaji hao waliipongeza serikali mkoani hapa kwa kutambua uwepo na umuhimu wao. Waliahidi kulifanyia kazi ombi la mkuu wa mkoa. Walisisitiza kuwa kila mtu anahitaji amani na utulivu ili kuyaendesha maisha yake.

Chanzo: habarileo.co.tz