Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chalamila ataka wananchi kulinda miundombinu

51118065dfea9b07c264b1e0b17b66b6 Chalamila ataka wananchi kulinda miundombinu

Fri, 26 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, amewataka wananchi wake kuwa walinzi wa miundombinu katika miradi ya maji inayopelekwa katika maeneo yao huku wakitambua na kuzingatia kuwa, lengo la serikali ni kuboresha maisha yao kwa kuwasogezea huduma.

Alisema hayo alipozungumza na wakazi wa Kijiji cha Lugombo, Kata ya Kandete katika Halmashauri ya Busokelo wilayani Rungwe akiwa ziara ya kukagua mwendelezo wa ujenzi wa Mradi wa Maji wa Mwakaleli I Skimu ya Ndala unayotekelezwa kwa akaunti ya dharura.

Alisema kumekuwa na kasumba ya baadhi ya watu kuhujumu miundombinu ya miradi ya maji, hatua inayorudisha nyuma jitihada za serikali kuwafikishia wananchi huduma bora za kijamii.

"Yapo baadhi ya maeneo hususani yaliyo na wafugaji, watu wanatumia mishale kutoboa mabomba yanayopitisha maji kupeleka kwa wananchi ili wanyweshe mifugo yao. Sasa kuna wakati tunafikiri na wao tutumie mishale hiyohiyo kuwatoboa ili tuwaulize kuna maumivu kiasi gani,” alisema mkuu wa mkoa.

Akaongeza: "Tutambue kuwa, serikali imedhamiria wananchi kuondokana na tatizo la maji... Vyanzo vya maji tunavyo, lakini maji hatujayaweka vizuri ili yafike kwa wananchi, wapo watu wachache wanaotaka kutukwamisha; tuseme hapana."

Awali, Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Usambazaji Maji Vijijini (Ruwasa), Paul Kambona, alisema mwanzoni mradi huo katika skimu ya Ndala ulikuwa unatekelezwa na mkandarasi, lakini baadaye ulichukuliwa na kutekelezwa na Ruwasa kwa usimamizi wa wilaya baada ya mkandarasi kusuasua.

Alisema Skimu ya Ndala ina vijiji vinane na mardi unatarajiwa kunufaisha wakazi 12,217.

Hadi sasa ujenzi wa chanzo umekamilika na sasa shughuli inayoendelea ni uchimbaji mitaro kwa ajili ya kuanza kulaza mabomba.

Alizitaja changamoto zinazokwamisha mradi huo kuwa ni pamoja na ubovu wa barabara kuelekea mahali kilipo chanzo cha maji unaosababisha kushindwa kufikisha mabomba kutokana na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha wilayani hapa.

Chanzo: habarileo.co.tz