Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chalamila ataka bei ya mkaa ipande

Mkaa33 Chalamila ataka bei ya mkaa ipande

Wed, 8 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema ili kuondokana na matumizi ya nishati chafu, basi ifike mahali bei ya gesi iwe chini na bei ya mkaa iwe juu.

Chalamila amesema hayo leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam ambapo imefanyika hafla ya uzinduzi wa Mkakati wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024 - 2034.

Chalamila ameongeza kuwa kutokana na idadi kubwa ya wakazi wa mkoa wa Dar-es-salaam kutumia mkaa, yeye ameungana na viongozi wa mikoa mbalimbali katika kutokomeza matumizi ya nishati chafu kwa kuhimiza watu wa mikoani kuacha kukata miti hovyo na wa mkoa wa Dar es Salaam kuacha kutumia mkaa kwa ajili ya kupikia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live