Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chalamila ashiriki usafi

Chalamila Chalamila ashiriki usafi

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila ameongoza zoezi la usafi leo January 24,2024 katika eneo la Maramba mawili, Mbezi akiwa na Viongozi na Wananchi wengine mbalimbali.

RC Chalamila aliitangaza siku ya leo kuwa ni ya usafi unaolenga kuwaepusha Wakazi wa Dar es salaam na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.

Asubuhi hii pia yanatarajiwa kufanyika maandamano yaliyoitishwa na CHADEMA ambapo RC Chalamila amewatoa hofu Wananchi kuwa usafi huo hauhusiani na maandamano yaliyoitishwa na CHADEMA na hautoathiri maandamano yao.

@AyoTV_ tayari ipo pia maeneo ya Buguruni na Mbezi ambako CHADEMA walitangaza kuwa maandamano hayo yataanzia na yakishaanza tutakupa ripoti ya kila kitakachojiri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live