Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chalamila akagua miradi ya maendeleo Kawe

Chalamila: Viongozi Wa Dini Muiombee Serikali Chalamila akagua miradi ya maendeleo Kawe

Fri, 23 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila leo amehitimisha ziara yake Wilaya ya Kinondoni katika jimbo la Kawe kwa kukagua miradi na kuzungumza na Wananchi eneo la Mabwepande-Kinondoni.

RC Chalamila katika ziara hiyo amefungua nyumba ya Mwalimu(2 in 1) Katika shule ya Sekondari Godwin Gondwe Kunduchi ambapo alipata wasaa wa kuzungumza na wanafunzi pamoja walimu wa Shule hiyo huku akiwataka wanafunzi kusoma kwa bidii kutokana na uwekezaji mkubwa ambao Rais Dkt Samia amefanya na anaendelea kufanya.

Aidha RC Chalamila pia amekagua mradi wa Hospital ya Wilaya ya Kinondoni- Mabwepande ambayo imejengwa kisasa inatoa huduma mbalimbali za Afya, vifaa tiba vya kisasa kwa sasa imeanza kutoa huduma za kuhifadhi maiti ambapo kwa siku inaweza kuhifadhi maiti 12 kwa wakati mmoja.

Vilevile RC Chalamila ametembelea kiwanda cha Smart Industry Limited kujionea uzalishaji na Changamoto ambapo amesema Serikali ya Mkoa inavutia uwekezaji wa ndani na nje kwa masilahi mapana ya wakazi wa Mkoa na Taifa kwa Ujumla

Sambamba na hilo RC Chalamila amefanya mkutano wa hadhara na Wananchi wa Mabwepande-Kinondo ambapo amesikiliza kero mbalimbali ikiwemo kero za urasimishaji wa Ardhi, migogoro ya Ardhi, Barabara, ufinyu wa huduma ya usafiri wa umma na nyingine nyingi ambapo kero nyingi zilizoibuliwa zilipatiwa majawabu papo hapo kwa kuwa katika ziara hiyo Mhe RC Chalamila ameambatana na wataalam wa sekta zote.

Pia RC Chalamila wakati wa mkutano huo wa hadhara amekabidhi vitendea kazi (Pikipiki) kwa jeshi la polisi na Bajaji kwa maafisa biashara wa Manispaa kwa ajili ya kukusanya Mapato.

Ifahamike kuwa Albert Chalamila ameridhishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika jimbo la Kawe-Kinondoni na amewataka viongozi wa Wilaya hiyo kuendelea kusikiliza na kutatua kero za wananchi, ambapo Februari 23, 2024 anatarajia kuendelea na ziara yake Wilaya ya Ubungo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live