Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chalamila afunguka kuhusu magonjwa yasiyoambukiza

Chalamila: Viongozi Wa Dini Muiombee Serikali Chalamila afunguka kuhusu magonjwa yasiyoambukiza

Tue, 31 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Imeelezwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa Mataifa yanayokabiliwa na changamoto ya magonjwa yasio ya kuambikiza, ambapo utafiti unaonesha katika kila vifo vitatu, kimoja kinatokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, hivyo ni muhimu kwa jamii kujenga utaratibu wa kupima afya zao mara kwa mara.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila, ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya wiki ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza kitaifa, yanayotarajiwa kufanyika jijini humo kuanzia Novemba mosi hadi 18 mwaka huu, yakiambatana na matukio mbalimbali ikiwemo utolewaji wa elimu na upaji wa magonjwa hayo.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dokta Rashid Mfaume, amesema ipo changamoto ya baadhi ya watu kutembea na maradhi bila kujua, na wanapofika hospitali wanafika wakiwa kwenye hatua mbaya za maradhi hayo, ikiwemo presha na Saratani, hivyo kupitia maadhimisho hayo, jamii itahimizwa na kuelimishwa kupima afya.

Maadhimisho hayo ya kitaifa ya wiki ya magonjwa yasio ya kubukiza yatafanywa kwa ushirikiano wa Wizara ya afya na ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam. ambapo yatatanguliwa na kongamano la kisayansi kuanzia Novemba mosi hadi tatu kwenye ukumbi wa Mwalomu Nyerere na kuanzia Novemba 11 hadi 18, kutakua na matamasha mbalimbali ya michezo yatakayoongozwa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dokta Jakaya Kikwete pamoja na utolewaji wa huduma za afya zifakazohitimishwa na Makamu wa Rais Dokta Philip Mpango kwenye viwanja vya mnazi mmoja Nobemba 19.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live