Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chalamila afungua mkutano wa wadau TIB

Chalamila: Viongozi Wa Dini Muiombee Serikali Chalamila afungua mkutano wa wadau TIB

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila, ameitaka Benki ya Maendeleo (TIB) kuendelea kuwezesha miradi ya uwekezaji hali, hatua ambayo amesema inachangia kuimarisha shughuli za maendeleo ya ukuaji wa Sekta mbalimbali za Kiuchumi hapa nchini.

RC Chalamila ametoa kauli hiyo alipokuwa akifungua Mkutano wa Wadau wa Benki ya Maendeleo TIB wa Kanda ya Dar es Salaam wenye lengo la kufanya majadiliano kati ya Benki na wadau wake.

Akifungua mkutano huo pia RC Chalamila amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake ya uwekezaji katika Benki hiyo.

"Kuendelea kukua kwa TIB kunatanua fursa za ajira kwa vijana wa kitanzania ambao wajipatia kipato na kuchangia katika kukuza uchumi wa Taifa" amesema RC Chalamila.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Bibi Lilian Mbassy amesema kuwa Taasisi hiyo inaendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuwezesha miradi ambayo inaleta ajira na kuchangia mapato ya serikali.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Agapiti Kobello amesema kuwa TIB itaendelea kukutana na wadau wake mara kwa mara kwa kuwa Suala la Huduma kwa Mteja, kwa Bodi ni suala la Kimkataba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live