Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chalamila afichua kero tatu Dar es Salaam

Chalamila: Changamkieni Fursa Mkutano Wakuu Wa Nchi Afrika Chalamila afichua kero tatu Dar es Salaam

Fri, 15 Sep 2023 Chanzo: mwanachidigital

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amemueleza Waziri Mkuu Kasim Majaliwa changamoto tatu zinazokabili mkoa huo.

Changamoto ambazo zinalikabili jiji hilo ni kelele, uzalishaji wa takataka na magonjwa yasiyoambukiza ambayo yanasababishwa kwa kiasi kikubwa na ulaji usio na mpangilio wa wakazi wa mkoa huo..

Ameyasema hayo leo Ijumaa, Septemba 15, 2023, jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa mpango mkakati wa Amref wa mwaka 2023-2030.

Amesema kutokana na uzalishwaji wa takataka kwa wingi katika jiji hilo, Amref waliamua kuelimisha wanawake ili kutumia fursa za kujipatia kipato kwa kubadilisha takataka na kuwa mkaa.

Chalamila amesema ujuzi huo umesababisha kupungua kwa takataka kwa baadhi ya maeneo na kutengeneza ajira kwa wingi.

Kwa upande mwingine mkuu wa mkoa huyo, amesema wananchi bado hawajajua umuhimu wa bima za afya hivyo, amewataka Amref waendelee kutoa elimu yenye msisitizo kuhusu umuhimu wa kuwa na bima za afya.

"Pale Hospitali ya Muhimbili, watu 150-180 wanakwenda kusafisha damu, ni gharama kubwa na wapo wasiokuwa na bima wanatumia gharama kubwa. Juzi kuna bodaboda kaingia katika uvungu wa mwendokasi tukatoa vipande hivyo elimu ya bima ni muhimu," amesema.

Huku pia akigusia umuhimu wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGOs) kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na madhumuni waliyoombea usajili.

"Kuna NGO's 2,400 ila kuna baadhi hazijulikani zinafanyakazi gani huku kukiwa na usajili wa makanisa nchi nzima 14600," amesema Chalamila.

Chanzo: mwanachidigital