Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chalamila: Tufanye kazi tuache visingizio

Chalamila Chalamila: Tufanye kazi tuache visingizio

Thu, 13 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amewataka wakazi wa Kagera kufanya kazi na kuacha visingizio kuwa umasikini wa mkoa huo umesababishwa na vita ya Kagera na ile ya Tanzania na Uganda

Ameyasema hayo leo wakati akitoa salamu zake katika hafka ya makabidhiani na uzinduzi wa Chuo cha Ufundi Stadi na Huduna cha Mkoa wa Kagera leo Alhamisi ya Oktoba 13, 2022 kilichojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya China.

Amesema baadhi ya wtu wamekuwa wakitembea barabarani na kusema mkoa huo hauna maendeleo kwa sababu Serikali haipeleki maendeleo.

"Sababu nyingine wanazotoa ni zile kuanzia Uhuru, Vita ya Kagera na kila kitu, wapo watu wanaosema mkoa huu umekuwa maskini kwa sababu ya vita ya Uganda na Tanzania, ninyi mnaolalamika wakati wa vita hiyo mlipigwa mabomu, mlitenguliwa miguu au vinginevyo," alihoji

"Naomba tukafanye kazi tuache visingizio, vyuo hivi vinakuja hapa tupeleke watoto wakasome," amesema Chalamila.

Chuo hicho kinaweza kuhudumua wanafunzi 400 wa kozi ndefu na wanafunzi 1000 wa kozi fupi huku kikigharimu Sh22 bilioni katika ujenzi wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live