Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chalamila: Nataka hela za barabara sio ma-blanketi

Chalamila: Changamkieni Fursa Mkutano Wakuu Wa Nchi Afrika Chalamila: Nataka hela za barabara sio ma-blanketi

Tue, 6 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila (@albert_john_chalamila) amesema amegomea kupokea misaada mbalimbali katika kipindi cha mafuriko hususani ile iliyotolewa kwa Wakazi wa mabondeni ikiwemo mablanketi na neti na badala yake anataka fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara.

Akiongea leo Jijini Dar es salaam wakati wa ukaguzi wa miundombinu mbalimbali amesema “Hizi barabara zetu inatakiwa tuzilinde zaidi kuliko hata kitu chochote na haya ndio maelekezo ya Mheshimiwa Rais wetu kwamba haya majanga yanapopatikana kwamba zamani ilikuwa ikitokea mafuriko tunaletewa mablanketi mwaka huu nimegoma sipokei blanketi sipokei neti wala kitu chochote nataka nipokee hela za kujenga barabara, hivyo wakapeleke Mufindi kwenye baridi ndio vikafanye kazi”

“Hapa kwa Dar es Salaam nataka mabarabara yetu yawe timamu, kuleta vituvitu fulani tutakuwa tunafurahia mafuriko, kwasababu tu mafuriko yamekuja tu kwenye nyumba eeeh sina ugali sina mboga kanywe maji kwa sababu umejenga kwenye maji”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live