Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chakula chaongeza ufaulu darasa la saba Songwe

C89cc8bc6e2c6c9dea3cfbe185336f53 Chakula chaongeza ufaulu darasa la saba Songwe

Sat, 19 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KUONGEZEKA kwa upatikanaji wa Chakula Cha mchana katika shule za awali na Msingi Mkoani Songwe Pamoja na usimamizi mzuri kwa pelekea kuongezeka kiwango Cha ufaulu matokeo Darasa la Saba.

Hayo yamebaainishwa na Afisa Elimu mkoa wa Songwe Juma Kaponda alipozungumza na gazeti hili ofisini kwake kujua hali ya upatikanaji wa Chakula na kiwango cha Ufaulu kilivyo ongezeka Mkoani Songwe.

Alisema upatikanaji wa Chakula Cha mchana kwa shule za Msingi na awali mkoa wa Songwe kumeongezeka kutoka shule 133 Mwaka 2019 mpaka kufikia shule 270 mwaka huu 2020 sawa na asilimia 63.

"Nichukue nafasi hii kumpongeza mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya na wasimamizi wote wa elimu kwa kulivalia njuga hili la kusisitiza kwa kukaa vikao na kuhakikisha shule zinatoa, jiografia ya Mkoa wa Songwe haiko vizuri kutokana baadhi ya Wanafunzi kutembea umbali mrefu wanapo kwenda shule hivyo kupatikana kwa chakula kunaongeza mahudhurio na kuimalisha ujifunzaji kwa Wanafunzi hao amao hutembea umbali mrefu " alisema.

Aliongeza, "Mwaka Jana 2019 ufaulu ulikuwa asilimia 75.51 lakini mwaka huu kiwango keep meongezeka na kufikia asilimia 78.92 ambapo ongezeko la ufaulu sawa na asilimia 3.21 , Jambo zuri zaidi kuongezeka kwa ufaulu wa daraja A na B tofaut na mwaka Jana ambapo ufaulu ulikuwa mdogo zaidi.”

Chanzo: habarileo.co.tz