Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema yataka Makonda ajiuzulu

15635 Makontena+pic TanzaniaWeb

Wed, 5 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kujiuzulu nafasi hiyo.

Pia, kimemtaka Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally kuweka bayana kwanini kiongozi huyo anakinzana na sheria za chama chake.

Akizungumza leo, katika mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa Ubunge wa Ukonga kupitia chama hicho, Asia Msangi, Naibu Katibu Mkuu Chadema-Zanzibar Salumu Mwalimu amesema jambo ambalo mkuu huyo wa mkoa amelifanya hivi karibuni hana sababu ya kuendelea na kazi hiyo.

Mwalimu amesema moja ya mambo ambayo CCM inasema inayasimamia ni uadilifu na kwamba inashangaa kwanini baadhi ya viongozi ndani ya chama hicho si waadilifu.

"Leo nataka nimwambie Katibu Mkuu (Dk Bashiru) atueleze mambo ambayo yanafinyangwa finyangwa, ndani ya CCM wapo wasio heshimu sheria, kanuni na Katiba, wasio waadilifu wapo," amesema Mwalimu.

Mwalimu alikuwa akizungumzia sakata la Makontena 20 yenye samani ambayo Makonda aliyaagiza na kuyaombea msamaha wa kodi ambao ulikataliwa.

"Makosa aliyofanya Makonda kwa nini bado yupo madarakani?” Alihoji Mwalimu.

Chanzo: mwananchi.co.tz