Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema kujenga kituo cha polisi Bashnet

Eyh Chadema kujenga kituo cha polisi Bashnet

Sat, 3 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MGOMBEA udiwani kata ya Bashnet mkoani Manyara kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mmao ameahidi kujenga kituo cha polisi cha kisasa kwa fedha za serikali tofauti na jengo la muda linalotumika akisema halina hadhi.

Mmao alisema hayo wakati akinadi sera na ilani ya chama chake mbele ya wapiga kura waliofika katika kampeni ya uchaguzi katika uwanja wa ofisi ya kata hiyo.

“Nichagueni mimi kuwa diwani wa kata ya Bashnet, mtaona mabadiliko makubwa ya maendeleo kuliko ilivyo hivi sasa. Kazi yangu ni kuitaka serikali kuu kutimiza haja hiyo,” alisema.

Alisema ameandaa vipaumbele katika kutatua kero za wananchi ikiwamo ya kutokuwa na kituo cha polisi kinachokidhi haja.

Kwa mujibu mgombea huyo, kituo kitakuwa na mahitaji yote ya muhimu ikiwamo chumba cha mashitaka, chumba cha kuhifadhi watuhumiwa wa kiume na wa kike pamoja na kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa Maji safi na salama na ya kutosha.

Alifafanua kuwa katika mkakati wa upatikanaji maji, yatavutwa kutoka chanzo cha maji cha Endalaa ambacho ni kikubwa kuliko vyote kilichopo kata ya Madunga cha Endalaa.

Kuhusu sekta ya afya alisema ataongeza upatikanaji wa dawa katika zahanati ya Bashnet, kituo cha afya cha Buma na ataviwezesha kuwa na wauguzi, madaktari, wahudumu vifaa, tiba na kinga vilevile kuboresha miundombinu ya hospitali hizo pamoja na mazingira yake.

Akimkaribisha mgombea kuzungumza na wananchi wa kata ya Bashnet kwenye mkutano huo, Katibu wa Jimbo wa Chadema, William Sarwatt aliwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura siku ya uchaguzi.

Chanzo: habarileo.co.tz