Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema: Tutasimama na watu wa Ngorongoro

Chadema Pic Ngoro Ngoro Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)-Tanzania Bara, Benson Kigaila

Sat, 11 Jun 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)-Tanzania Bara, Benson Kigaila amesema chama hicho kipo pamoja na watu wa Ngorongoro dhidi ya changamoto wanazozipitia katika siku hizi za karibuni.

Kigaila ameyasema hayo leo Juni 11, 2022 wakati wa mahafali ya Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu ambao ni wanachama wa Chadema (Chaso) kutoka vyuo vilivyopo jijini Dar es Salaam yaliyofanyika katika makao makuu ya chama hicho Kinondoni.

Amesema watu wa Ngorongoro wanayo haki ya kukaa katika ardhi hiyo kisheria, hivyo Serikali iache oparesheni ya kuwaondoa watu katika maeno ya Ngorongoro.

"Sisi kama Chama tutasimama na watu wa Ngorongoro hivyo Serikali inatakiwa itambue hilo" amesema

Kigaila amesema Serikali inatakiwa itoe ufafanuzi wakina na kuwajulisha Watanzania kuwa Ngorongoro kuna uwekezaji gani unaotaka kufanyika.

"Serikali iwaeleze wa Tanzania kuna jambo gani linafanyika Ngorongoro kama sio uvunaji" amesema

Amesema kuwa Bunge, linatakiwa liunde kamati ili waende wakachunguze madhara yaliyotokea Ngorongoro.

Leo mapema Mkuu wa Mkoa Arusha, John Mongella alisema kuwa askari mmoja alifariki dunia baada ya kushambuliwa kwa kupigwa mshale na kundi la watu wenye silaha wakati wa zoezi la uwekaji wa alama za mipaka katika eneo la Loliondo wilayani Ngorongoro.

Pia, Mongella alisisitiza kuwa hali ya Loliondo ni shwari na uwekezaji wa mipaka katika eneo la kilometa 1,500 kwa ajili ya eneo nyeti la mazalia, chanzo cha maji na mapito ya wanyama kwenye eneo hilo.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz