Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CWT watoa mifuko 300 ya saruji ujenzi wa miundombinu ya shule Dodoma

78478 Pic+cwt

Fri, 4 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma.  Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimekabidhi mifuko 300 ya saruji katika ofisi ya Jiji la Dodoma kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu katika shule za msingi, ikiwa ni pamoja na upungufu wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu.

Akizungumza leo Ijumaa Oktoba 4, 2019 wakati wa kukabidhi mifuko hiyo katibu mkuu wa CWT, Deus Seif amesema msaada huo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha sekta ya elimu nchini.

Amesema mjini Dodoma madarasa kwa shule za msingi ni asilimia 37.5, kwamba mchango huo ni sehemu ya kupunguza changamoto ya upungufu wa matundu ya vyoo, madarasa pamoja na nyumba za waalimu.

“Ili mwalimu afundishe vizuri anahitaji kuwa na makazi bora, ili mwanafunzi aweze kupata elimu bora ni lazima atengenezewe mazingira bora, hiyo ikatusukuma kutoa mchango huu na ni mwanzo tu,” amesema Mwalimu Seif.

Awali, ofisa elimu msingi mjini Dodoma, Joseph Mabeyo amesema Halmashauri ina wanafunzi wa shule za msingi 97,526  ambao wanahitaji vyumba vya madarasa 1,522 wakati vilivyopo ni 916.

Amesema wanahitaji yumba za walimu 1776, kwamba  zilizopo ni 167 sawa na upungufu wa nyumba 1610.

Pia Soma

Advertisement
Mahitaji ya matundu ya vyoo vya wavulana ni 1936 yaliyopo ni 509 na upungufu ni 1427, na kwa wasichana mahitaji ni matundu 2456, yaliyopo ni 577 na upungufu ni 1879.

“Hali hii imesababisha halmashauri ya Jiji la Dodoma kutafuta wafadhili mbalimbali ili kutoa hisani kuwezesha vifaa vya ujenzi kwa lengo la kupunguza changamoto ya upungufu wa miundombinu ya sekta ya elimu tukawapata CWT ambao wametoa mifuko 300 ya saruji,”  amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz