Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

COVID - 19 yapunguza abiria KIA

Kilimanjaro Airpot.jpeg Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: eatv.tv

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya uendelezaji wa kiwanja cha ndege cha Kilimanjaro (KIA) Christine Mwakatobe amesema Mlipuko wa UVIKO 19 ulisababisha kushuka kwa kiwango cha abiria  kutoka 794,337 mwaka 2019/2020 hadi 347,757 katika kipindi cha mwaka 2020/2021

Bi. Mwakatobe amesema kutokana na janga hilo wamechukua hatua za haraka kunusuru pato la uwanja huo lisishuke.

Katika hatua nyingine Mwakatobe amesema Filamu ya Royal Tour iliyoigizwa na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ya kuitangaza nchi imeongeza mapato kwa abiria kutoka 347,757 Mwaka 20209/2021 na kufikia abiria 654,159 Mwaka 2021/2022 hii ni sawa na ongezeko la asilimia 88

Kuhusu usafirishaji wa nyama Mwakatobe amesema kwa juhudi zilizofanywa na Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan zakuinua democrasia ya kiuchumi imeongeza soko la nyama hasa ikiwa ni kipindi cha kuelekea kombe la Dunia.  

Chanzo: eatv.tv