Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yazungumzia zuio la mifuko ya plastiki

61329 Ccmpic

Tue, 4 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeipongeza Serikali kwa kufanikisha kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki na kuahidi kushiriki katika kuhakikisha mifuko hiyo inatokomea kabisa.

Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Erasto Sima ameyasema hayo leo Juni 4, 2019 wakati akikabidhi kompyuta na mashine ya kurudufu kwa makatibu wa chama hicho katika mikoa ya Tanga, Dar es Salaam na Pwani.

Amesema jumuiya hiyo inafahamu umuhimu wa katazo la mifuko ya plastiki na itaendelea kuwahamasisha Watanzania kwenye matumizi ya vifungashio na mifuko mbadala.

Kuhusu vifaa hivyo alivyokabidhi Sima amesema ni utekelezaji wa ahadi ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Najma Giga aliyoitoa kwa ofisi zote za jumuiya ya wazazi.

“Mbunge aliahidi na ametekeleza ahadi yake kwa vitendo, hadi sasa ametoa kompyuta na mashine za photocopy kwa mikoa 27 na wilaya zote 12 za Zanzibar huku akiwa amesaliwa na mikoa mitano tu,” amesema

“Nitumie fursa hii kumuomba Mbunge mwenzie wa viti maalum aliyetokea jumuiya ya wazazi kuiga mfano huu, asaidie kwa namna yake kwa kuwa hawa wote ni wabunge,” amesema

Pia Soma

Sima ameeleza kuwa hadi sasa Giga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge ametoa vifaa vinavyogharimu Sh44 milioni.

Akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo Katibu wa jumuiya wa wazazi mkoa wa Tanga, Hassan Mdoe amesema msaada huo utawawezesha kutunza siri za chama.

“Tulikuwa tunalazimika kwenda kuchapa au kurudufu kwenye maeneo ya watu binafsi na hapo ndipo siri za chama zilipokuwa zinaanzia kuvuja, lakini kwa msaada huu sasa kila kitu kitafanyika ndani ya ofisi,” amesema

Chanzo: mwananchi.co.tz