Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CCM yaiomba Serikali ya Tanzania kudhibiti uzalishaji wa vikobo Iringa

Fri, 20 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Iringa. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Iringa, Abel Nyamahanga ameiomba Serikali ya Tanzania na mamlaka husika kuhakikisha wanapunguza kasi ya uzalianaji wa viboko katika Bwawa la Mtera ili kuokoa vifo na maisha ya wananchi waishio katika eneo hilo.

Nyamahanga amesema hayo leo Ijumaa Septemba 20,2019 katika maadhimisho ya utalii wa Nyanda za Juu Kusini ‘Karibu Kusini’ wakati akitoa salamu za chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa.

"Naiomba Serikali na mamlaka husika kudhibiti uzalianaji wa viboko kwa sababu wamekuwa wengi na wanahatarisha maisha ya wananchi na kusababisha vifo," amesema

Pia, Nyamahanga ameiomba Serikali kukarabati kambi ya wapigania uhuru ya Kihesamgagao iliyopo Wilayani Kilolo mkoani humo na kuigeuza kuwa sehemu ya makumbusho ili kuvutia watalii.

Amesema kambi ya Kihesamgagao kwa sasa imegeuzwa kuwa gereza jambo ambalo limeifanya historia ya eneo hilo kupotea.

"Tunaomba Kambi ya Kihesamgagao pageuzwe kuwa sehemu ya makumbusho, nimepata taarifa kwa sasa kuna wafungwa 16 na watoto zaidi ya 400 waliozaliana kutokana na ujio wa wapigania uhuru hivyo kwa kuwekwa kumbukumbu tunaweza kutengeneza kivutio kizuri kwa watalii," amesema

Pia Soma

Advertisement
Mbali na hayo, Nyamahanga amesema Iringa ina kabila moja la Wahehe ambalo ni utalii tosha.

"Katika Mkoa wa Iringa Kalenga ni eneo ambalo kuna kichwa cha mwanaume (Chifu Mkwawa) ambaye alipambana na wanaume limehifadhiwa pale," amesema

Maadhimisho hayo yanafanyika kwa siku tatu kuanzia leo hadi keshokutwa Jumapili Septemba 22,2019 yatakapofungwa. Mikoa inayoshiriki katika maadhimisho hayo ni Morogoro, Iringa, Rukwa, Katavi, Mbeya, Ruvuma, Songwe na Njombe

Chanzo: mwananchi.co.tz