Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"CAR WASH" zafungwa Shinyanga

WhatsApp Image 2021 10 14 At 6.16.30 AM.jpeg "CAR WASH" zafungwa Shinyanga

Thu, 14 Oct 2021 Chanzo: ippmedia.com

 MKURUGENZI wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, ametoa ufafanuzi juu ya sintofahamu ambayo imetokea ya kufungwa kwa baadhi ya vituo vya kuoshea Magari (CAR WASH) Mjini humo na kusababisha watu kukosa huduma za kuosha magari yao.

Akizungumza na Nipashe leo, amesema wamefunga vituo hivyo vya kuoshea Magari, sababu ya kutofuata taratibu za Serikali na kuweka vituo hivyo holela na kuharibu mipango mji.

Amesema walifanya Oparationi ya kukagua vituo vyote vya kuoshea Magari Manispaa ya Shinyanga, na kubaini wamiliki wake hawakufauta utararibu wa Serikali kwa kupewa vibali na Afisa mipango miji, bali wameingia mikataba na wamiliki wa maeneo kitendo ambacho ni kinyume na utaratibu, na kulazimika kuvifunga.

 “Manispaa ya Shinyanga tuna mpango wa kuutengeneza Mji kuwa hadhi ya Jiji, hivyo kutokana na kuwapo kwa vituo vingi vya kuoshea Magari holela, bila ya kupata vibali kutoka Halmashauri kwa Afisa Mipango Miji nikaagiza wavifunge vyote na kufuata utaratibu,”amesema Satura.

“Hatuwezi kuwa na mji ambao hauna mpangilio, Manispaa ya Shinyanga ndiyo wenye mamlaka ya upangaji mji, lakini unakuta Mfanyabiashara ameingia mkataba na Shirika la Reli (TRC), Wakala wa Barabara (TANROADS) au mtu ana kiwanja chake ana sehemu kwa mbele inawekwa CAR WARSH hilo hatulitaki bali wafike Halmashauri wapewe utaratibu,”ameongeza.

Aidha ,amesema hawajafunga vituo hivyo vya kuoshea Magari kwa maksudi, sababu wanafahamu vimetoa ajira nyingi kwa vijana, bali wanachotaka ni kufuatwa kwa utaratibu wa Serikali juu ya mipango miji, kwa kupata kibali na kuonyeshwa maeneo sahihi ya shughuli hizo, na siyo kuweka kila mahari na kuharibu Mji.

Nao baadhi ya wafanyabiashara ambao wanamiliki vituo hivyo vya kuoshea magari, walilalamika kufungiwa vituo vyao ghafla bila ya kupewa maelekezo yoyote, huku wakipewa siku Tano hadi siku ya jumatatu, wawe wameshafika kwenye Ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupewa utaratibu wa Serikali.

Chanzo: ippmedia.com