Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bweni lingine lateketea Geita

Bweni Geita Moto.png Bweni lingine lateketea Geita

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Moto ambao chanzo chake hakijajulika umeteketeza bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari ya Marry Queen of Peace mjini Geita.

Janga hilo moto limetokea Saa 8:00 mchana Oktoba 23, 2023 wakati wanafunzi wakiendelea na shughuli za kawaida za kimasomo.

Licha ya kutekeza samani na mali za wanafunzi, moto huo pia imesababisha madhara ya mshtuko kwa baadhi ya wanafunzi.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Geita, Hamis Dawa amesema askari wa jeshi hilo kwa kushirikiana na wadau wengine wamefanikiwa kuudhibiti moto huo kabla ya kusababisha madhara makubwa.

“Tunaendelea na uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha moto huo," amesema Kamanda Hamisi

Amesema pamoja na vifaa vya masomo, moto huo pia umeteketeza vitanda na magodoro, ndoo na mali binafsi za wanafunzi.

Amesema Jeshi hilo limekuwa likitoa maelekezo kwa wamiliki wa taasisi zenye idadi kubwa ya watu kuweka miundombinu ya kuwezesha watu kijiokoa wakati wa majanga ikiwemo milango ya dharura.

Goreth Cosmas, mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo amesema japo wanamshukuru Mungu kwa kuepusha madhara kwa maisha ya binadamu, tukio hilo limeibua hofu miongoni mwao.

Katibu wa Askofu Jimbo Katoliki Geita inayomiliki Shule hiyo, Padri Yohane Mabula amesema moto huo umesababisha hasara ambayo thamani yake hiajajulikana hadi tathmini itakapofanyika.

"Tunamshukuru Mungu hakuna madhara makubwa kwa binadamu zaidi ya mshtuko na majeraha madogo madogo wakati wa jitihada za uokoaji. Kuhusu hasara ni hadi tutakapokamilisha ukaguzi na tathmini ya mali yote iliyoteketea," amesema Padre Mabula

Chanzo: www.tanzaniaweb.live