Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bweni lateketea kwa moto Songwe

NYUMBA BWENI MOTO Bweni lateketea kwa moto Songwe

Fri, 14 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Moto ambao chanzo chake bado hakijafahamika umeunguza bweni la Wanafunzi 64 katika Shule ya Sekondari Vwawa iliyopo Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Songwe, Elautery Mremi amesema moto huo umeanza leo Ijumaa Aprili 14, 2023 asubuhi ambapo Jeshi hilo limefanikiwa kuudhibiti usienee kwenye mabweni mengine na madarasa.

Kamanda huyo amesema kuwa hakuna majeraha wala vifo vilivyosababishwa na moto huo huku tathmini ikiendelea kubaini madhara na chanzo cha moto huo.

Kamanda Mremi amesema bweni hilo lilikuwa linatumiwa na Wanafunzi 64 ambapo vitu vilivyokuwemo ndani ya bweni hilo vimeteketea, wakati moto huo unatokea Wanafunzi walikuwa darasani wakiendelea na mitihani.

Kamanda Mremi amesema changamoto iliyotokea ni Jeshi hilo kupata taarifa kwa kuchelewa huku akitoa wito kwa Uongozi wa Shule ambazo zina mabweni kuweka Walinzi muda wote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live