Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bwawa la Mtera hatarini kukauka, kaya 300 huhama

Bwawa Mtera Wed Bwawa la Mtera hatarini kukauka, kaya 300 huhama

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya kaya 300 katika kijiji cha Mnadani katika Halmashauri ya wilaya ya Iringa zilizopo ndani ya hifadhi ya bwawa la Mtera zimetakiwa kuhama ili kunusuru bwawa hilo ambalo liko hatarini kutoweka kutokana na kuathiriwa na shughuli za kibinaadamu ikiwemo kilimo

Bwawa la mtera limekuwa tegemeo kwa wakazi wa halmashauri za wilaya ya iringa, chamwino na Mpwapwa kwa ajili ya kufanya shughuli za uvuvi na kuendesha miasha yao lakini changamoto kubwa kwasasa bwawa hilo maji yake yanazidi kupungua na samaki kutoweka kutokana na wananchi wanaozunguka bwawa hilo kufanya shughuli za kilimo pembezoni mwa bwawa hilo

Lakini katika kunusuru bwawa hilo Tume ya taifa ya mipango ya matumizi ya ardhi kwakushirikiana na ofisi ya makamu wa rais Mazingira imeanza utekelezaji wa mradi wa uhifadhi wa vyanzo vya maji kwenye vijiji vya makuka ,makatapola na mnadani wilayani iringa ambavyo vinavyozunguka bwawa hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live