Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bustani ya Milioni 70 kutengeneza Geita

GTAA Bustani ya Milioni 70 kutengeneza Geita

Sat, 5 Dec 2020 Chanzo: millardayo.com

Zaidi ya Milioni 70 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa bustani ya kupumzikia kwa wakazi wa mji wa Geita ili kuwapa fursa ya kuwa na eneo la kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo kupumzika, kupunga upepo pamoja na kuepuka kero za joto.

Mradi huo unaotekelezwa na Halmashauri ya Mji Geita. kushirikiana na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), umefadhiliwa na kampuni hiyo kwa kupitiua fedha za mfuko wake wa uwajibikaji wa kwa Jamii (CSR).

Akizungumza katika hafla ya kuzindua ujenzi wa bustani hiyo katika kata ya Kalangalala mjini Geita, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel alisema mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi huu.

Alisema mradi huo unaotekelezwa katika eneo la mita za mraba 4000 katika kata ya Kalangalala mjini Geita, una lengo la kuwapatia wakazi wa Mji wa Geita fursa ya kuwa na eneo la kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo kupumzika, kupunga upepo pamoja na kuepuka kero za joto.

“Lengo letu ni kuona wakazi wa Mji wa Geita wanafika katika eneo hili kufurahia upepo asilia sanjari na kuona mnara maalum wenye kumbukumbu ya Mkoa wa Geita, bustani hii itakuwa kivutio pia kwa vile inajengwa kwa tofali za kuvutia kwenye maeneo yote ya kupitia na sehemu za watu kuketi hali ambayo itashawishi watu wengi zaidi kukaa na kujionea uzuri wa Mji wetu wa Geita,” Mkuu huyo wa Mkoa.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Richard Jordinson alisema kuwa Kampuni ya GGML imekuwa ikifanya jitihada kubwa kubadilisha muonekano wa jamii ya Mkoa wa Geita kwa kuanzisha miradi endelevu. 

“GGML tunajivunia kuwa, wakati tunasherehekea miaka 20 ya uwekezaji wetu ndani ya Mkoa wa Geita mwaka huu, tumefanikiwa kutekeleza miradi mingi yenye tija na matokeo chanya ikiwemo mnara wa makutano ya barabara Mjini Geita, masoko, taa za barabarani, vituo vya afya, shule na barabara za lami,” Richard Jordinson.

Chanzo: millardayo.com