Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunduki tano zakamatwa zikikodishwa na risasi 300

Bunduki Bunduki tano zakamatwa zikikodishwa na risasi 300

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kukamata bunduki tano ambazo wamiliki wake walikuwa wamezikodisha kwa makampuni kinyume cha utaratinbu.

Hayo yamesemwa leo Jumatano, Julai 26, 2023 na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP-Leonard Nyandahu wakati akitoa taarifa ya mwezi kuhusu matukio ya uhalifu na hali ya usalama mkoani humo baada ya oparesheni maalum walioifanya.

“Katika Oparesheni hiyo tumeweza kukamata bunduki tano, rifles nne, na Mark 4 moja, pamoja na risasi za shortgun na pistol, zaidi ya 300.

"Bunduki hizi wamiliki wake wanazimiki kwa halali lakini wanazikodisha kwa watu wengine jambo ambalo ni kinyume cha sheria. Kama unamiliki bunduki miliki wewe na uitumie wewe mwenyewe, kwa matumisi yako na si kukodisha.

"Kwa hiyo tutaangalia namna ya kuwashughulikia hawa waliokuwa wakizikodisha. Tulipata taarifa pia kuwa kuna mahali risasi zimefichwa, tulipopekuwa tukazikuta na tumezichukua ziko hapa," amesema Kamanda Nyandahu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live